|  | 
| Pichani ni bishost mrembo mwenye uraibu wa michoro ya tattoo akionyesha swag | 
Ebu
fikiria kwa makini, ni sawa kwa mtu kuwa na shati moja maisha yake yote? Mmh
utakuwa sahihi kabisa endapo jibu lako litakuwa si sawa kimtazamo wa wengi.
Naam! hivyo ndivyo namna  michoro mwilini "tattoo" ilivyo, unachorwa mwili kwa wino usioweza
kufutika kirahisi hivyo  alama/mchoro
hubaki mwilini mwako daima. Kwa lugha ya kigeni michoro hii hujulikana kama
“tattoo” kwani hutokana na neno la “kitahiti” litamkwalo “tatu” kwa maana
ya  alama ya kudumu inayobuniwa na
kuchorwa kwenye  ngozi kwa kutumia rangi
za aina mbalimbali. Siku hizi michoro hii huchorwa kwa kutumia sindano na kifaa
cha kisasa cha umeme chenye sindano kinachotoboa tabaka la juu la ngozi (dermal layer)
kirahisi na kufanya mchoro au alama za aina Fulani. Vifaa hivi kitaalamu tunaviita "rapid-injection-electronical device". Katika insha hii
nitabainisha kwa kina madhara yaletwayo na michoro hii ambayo imepewa
kipaumbele na jamii ya sasa hosusani vijana. 
Ndiyo waweza kupata madhara 
kiafya, kimtazamo wa jamii inayokuzunguka, na hasara zisizo za lazima
kiuchumi.
Athari Kiafya
Athari Kiafya
Afya
bora ni muhimu sana sana 
Tatizo
lingine la michoro hii ni mtazamo hasi kutoka kwa jamii inayopinga michoro na nembo za aina
hii. Kumekuwepo na uvumi kutoka kwa jamii kuhusu makundi ya watu wanaochora
michoro hii kuwa ni wale wanaojihusisha na vitendo viovu vya kinyama, kihuni au kikatili. Katika ofisi mbalimbali za kazi waajiri hukataa kutoa ajira kwa watu
wenye michoro na nembo hizo. Kumekuwepo na visa vya wazazi kuwakataa watoto wao
kwa kuwa wamejichora michoro hiyo. zipo baadhi ya sehemu za kujipatia huduma
ambazo haziruhusu wateja wake kuingia huku wakeka wazi michoro hiyo; mfano
katika mikahawa ya vyakula na hoteli mbalmbali duniani.
Athari za Kiuchumi
Athari za Kiuchumi
Kwakweli
michoro hii ikifuata taratibu za kiafya zinazo kubalika mchorwaji hulazimika
kutoa fedha nyingi kuliko maelezo. Studio nyingi zimeonyesha takwimu za gharama
ya kuchora michoro hiyo kwa saa moja ni zaidi ya $100 (Dola mia moja) hivyo
ukihitaji tatoo kwa masaa manne au zaidi ni fedha nyingi mno. Zipo gharama
zinazolipwa ikiwa mchoro umemsababishia mhusika maambukizi. Hizi ni gharama za
kununua madawa ya kutibu ngozi (vidonda).

 
 
No comments:
Post a Comment